Posts

  Hesabu 23:19 inasema: “ Mungu si mtu, aseme uongo; wala si mwanadamu, ajute. Je! Yeye alisema, naye hatalitenda? Au amenena, naye hatalitimiza ?” Maana yake kwa ufupi Aya hii inatufundisha kwamba Mungu ni mwaminifu na habadiliki kama wanadamu . Anaposema jambo, ana uwezo na uaminifu wa kulitenda na kulitimiza.

MASOMO YA MISA, JUMATATU, AGOSTI 11, 2025 JUMA LA 19 LA MWAKA

  MASOMO YA MISA,  JUMATATU, AGOSTI 11, 2025 JUMA LA 19 LA MWAKA  Kumbukumbu ya Mtakatifu Klara SOMO 1 Kum 10: 12-22 Sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri? Tazama, mbingu ni mali za Bwana, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vili- vyomo. Tena, Bwana aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo. Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu. Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiye- pendelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa. Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. Basi, mpende...