Monday, May 29, 2017

MTANZANIA MWENYE UMRI MDOGO AHITIMU PhD YA UCHUMI NCHINI SWEDEN

Mtanzania Martin Chegere (30) ameweka rekodi ya kuwa mmoja ya Watanzania wenye umri mdogo zaidi kuhitimu Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Uchumi. Martin alipitishwa jana na Chuo Kikuu cha Gothenburg nchini Sweden. Mafanikio ya Martin katika ku×kia kiwango hicho cha elimu kwa umri humo mdogo umepongezwa na wengi kutokana na ukweli kwamba ni kazi ngumu kwa nchi za kiafrika ku×kia kiwango hicho katika umri mdogo namna hiyo kutokana na mfumo wa elimu na maisha kwa ujumla.

Martin Chegere ambaye sasa anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Idara ya Uchumi, alisoma Shahada Uzamivu (PhD) katika vyuo viwili vya UDSM Tanzania na kile cha Gothenburg nchini Sweden. Chegere amekuwa na historia nzuri katika maisha yake ya kitaaluma ambapo matokeo ya kidato cha nne mwaka 2004 aliibuka na kushika namba moja kwa ufaulu nchini (Tanzania One). Elimu yake ya sekondari alisoma Maua Seminary mwaka 2001 hadi 2004 mkoani Kilimanjaro.

Aliendelea na elimu ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Pugu kati ya mwaka 2005 hadi 2007 ambapo alipohitimu mwaka 2007 alishika nafasi ya kwanza kwa ufaulu (Tanzania One) katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita. Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alisoma Shahada ya Awali (Bachelor Degree) katika Uchumi kuanzi mwaka 2007 na kuhitimu 2010. Baada ya hapo aliendelea na masomo katika Shahada ya Umahiri (Masters Degree) ambapo alihitimu mwaka 2012 katika Uchumi.


Licha ya kuwa amejikita zaidi katika masuala ya uchumi, lakini ni mbobezi pia kwenye Economics of climate change, Adaptation and mitigation na Risk, shocks and poverty issues Martin Shegere alizaliwa Oktoba mwaka 1986 lakini pia, ameoa mke mmoja na ana mtoto mmoja.


Source: swahilitimes


HONGERA NYINGI SANA KWAKE!

No comments: